Deuteronomy 5:23-27

23 aMliposikia sauti kutoka kwenye giza, mlima ulipokuwa ukiwaka moto, viongozi wenu wote wa makabila yenu na wazee wenu walinijia mimi. 24 bNanyi mkasema, “Bwana Mwenyezi Mungu wetu ametuonyesha utukufu na enzi yake, nasi tumesikia sauti yake kutoka kwenye moto. Leo tumeona kwamba mwanadamu anaweza kuishi hata kama Mungu akizungumza naye. 25 cLakini sasa, kwa nini tufe? Moto huu mkubwa utatuteketeza sisi na tutakufa kama tukiendelea kusikia sauti ya Bwana Mwenyezi Mungu wetu zaidi. 26 dNi mtu yupi mwenye mwili ambaye amewahi kuisikia sauti ya Mungu aliye hai akizungumza kutoka kwenye moto, kama sisi tulivyoisikia, naye akaishi? 27 eSogea karibu usikie yale yote asemayo Bwana Mwenyezi Mungu wetu. Kisha utuambie chochote kile ambacho Bwana Mwenyezi Mungu wetu anakuambia. Tutasikiliza na kutii.”

Copyright information for SwhKC